1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Mkuu wa NATO asema Ukraine bado haijachelewa kushinda vita

29 Aprili 2024

Mkuu wa jumuiya ya kujihami ya NATO Jens Stoltenberg, amesema Ukraine "haijachelewa" kushinda vita dhidi ya Urusi, wakati akikubaliana na Rais Volodymyr Zelensky kwamba Kyiv inahitaji silaha zaidi.

https://p.dw.com/p/4fJVa
Ukraine | Volodymyr Zelenskyy na Stoltenberg mjii Kyiv
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg akiwa na Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine mjini Kyiv.Picha: Efrem Lukatsky/AP Photo/picture alliance

Katika mkutano wa wanahabari nchini Ukraine Stoltenberg amesema Ukraine imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa silaha kwa miezi kadhaa, lakini hajachelewa kujiimarisha na kupata ushindi kwani msaada zaidi uko njiani.

"Kwa miezi kadhaa, Marekani haikuweza kukubaliana kuhusu kifurushi cha msaada kijeshi, na washirika wa Ulaya wameshindwa kutoa silaha kwa kiwango tulichoahidi. Ukraine imekuwa na uhaba wa silaha. Hii hiyo ina maana kwamba makombora machache na droni za Urusi zimedunguliwa na Urusi imepata mafanikio makubwa kwenye mstari wa mbele wa vita. Lakini bado Ukraine haijachelewa kushinda. Msaada zaidi uko njiani," amesema Stolteberg.

Akizungumzia msaada uliosubiriwa kwa muda mrefu, Zelensky alisema baadhi ya "vitu" vimeanza kuwasili lakini alikataa kutoa maelezo zaidi.