1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Wapalestina zaidi ya laki tano hawana makazi Gaza

Saumu Mwasimba
14 Mei 2024

Umoja wa Mataifa wasema zaidi ya Wapalestina Nusu milioni wameachwa bila makaazi kufuatia mashambulizi ya Israel Kusini na Kaskazini mwa Gaza.

https://p.dw.com/p/4fq80
Ukanda wa Gaza | Wapalestina wanaondoka Rafah
Wapalestina wanasafirisha mali zao wakikimbia Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza kuelekea eneo salama Mei 12, 2024.Picha: -/AFP

Kwa mujibu wa shirika la Umoja huo linalowasaidia wakimbizi wa kipalestina-UNRWA, takriban Wapalestina 450,000 wamelazimika kuondoka kwenye mji wa Rafah ulioko Kusini mwa Gaza katika kipindi cha zaidi ya wiki moja iliyopita. Watu wasiopunguwa milioni 1.3 walikuwa wakiishi katika mji huo kabla ya Israel kuanza kuingia kuendesha operesheni zake.

Israel inasema Rafah ni ngome ya mwisho ya wanamgambo wa kundi la Hamas. Maafisa wa Palestina wamesema mashambulizi ya Israel katikati mwa Gaza yamewauwa kiasi watu 12 usiku wa kuamkia leo Jumanne.

Wakati huohuo jeshi la israel limesema gari lililokuwa limewabeba wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa ambalo limeshambuliwa kusini mwa Gaza lilikuwa katika eneo linalokabiliwa na mapambano wakati watukiohilo.Umoja wa Mataifa umesema afisa wake mmoja wa  usalama ameuwawa katika tukio hilo.