1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Waziri Kiongozi wa Scotland atangaza kujiuzulu

29 Aprili 2024

Waziri kiongozi wa Scotland Humza Yousaf amejiuzulu leo Jumatatu, kabla ya kura mara mbili za kutokuwa na imani naye ambazo zingeweza kuiangusha serikali yake inayoongozwa na Chama cha Scotland National Party (SNP).

https://p.dw.com/p/4fJVZ
Scotland| Edinburgh 2024 | Humza Yousaf
Waziri Kiongozi wa Scotland Humza Yousaf ametangaza kujiuzulu kutokana na shinikizo la kisiasa.Picha: Andrew Milligan/REUTERS

Uongozi wa Yousaf uliingia matatani wiki iliyopita alipofuta makubaliano ya ushirikiano kati ya Chama chake SNP na Chama cha Kijani cha Scotland.

Kiongozi huyo amesema "alipuuza" maumivu aliyosababisha kwa kusitisha bila kujali makubaliano ya SNP ya kugawana madaraka na chama cha Kijani katika bunge la Scotland wiki iliyopita.

Yousaf ameiongoza Scotland kwa miezi 13 pekee, baada ya Nicola Sturgeon kutangaza ghafla kujiuzulu baada ya miaka minane ya uongozi.

Bunge la Scotland sasa lina siku 28 kuchagua kiongozi mpya.