1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama Ujerumani yaelezwa mipango ya njama ya mapinduzi

29 Aprili 2024

Waendesha mashtaka nchini Ujerumani, wameifahamisha mahakama ya mjini Stuttgart, kwamba watu wanaotuhumiwa kupanga njama ya mapinduzi dhidi ya serikali ya Ujerumani walikuwa wamepiga hatua katika mipango yao.

https://p.dw.com/p/4fJVb
Stuttgart | Watuhumiwa wa njama ya mapinduzi
Watuhumiwa wa njama za kuipindua serikali ya Ujerumani wakifikishwa mahakamani mjini Stuttgart. Picha: Bernd Weißbrod/dpa-Pool/picture alliance

Imeelezwa kwamba tayari walikuwa wamekamilisha mipango ya kuanzisha muundo wa kijeshi wa taifa kupambana na upinzani wowote dhidi yao. 

Wakati wa kusikiliza kesi dhidi ya washukiwa tisa wa vuguvugu la siasa kali za mrengo wa kulia linalojiita  "Reichsbürger" waendesha mashtaka wamesema nia ya watuhumiwa  kutumia vurugu ilidhihirishwa na mmoja wao Markus L, alivyofyatua risasi dhidi ya polisi wakati wa kumkamata na kumjeruhi polisi mmoja wakati wa makabiliano hayo.

Kesi hii ni ya kwanza kati ya tatu inayowahusu washukiwa 27 wanaotuhumiwa kula njama ya kupindua serikali ya shirikisho ya Ujerumani, iliyotibuliwa na mamlaka mwishoni mwa mwaka 2022.